Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

``Hakuna aliyeweza kukitegua kitendawili chenyewe lakini…’’
a)Eleza muktadha wa dondoo hili. ( alama 4)
b) Tambua tamathali ya usemi iliyotumiwa katika dondoo hili. (alama 2)
c) Fafanua chanzo na hatima ya kitendawili kinachorejelewa katika dondoo hili. (alama 10)
d) Eleza wasifu wa warejelewa katika dondoo hili. ( alama 4)

 (8m 27s)
4572 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
``Hakuna aliyeweza kukitegua kitendawili chenyewe lakini…’’
a)Eleza muktadha wa dondoo hili. ( alama 4)
i) hii ni kauli ya mwandishi
ii) anarejelea tukio la ulafi wa Jitu
iii) mahali ni katika mkahawa mshenzi wa Mzee Mago
iv) watu wamepigwa na butwaa kwa tendo la ulafi wa Jitu
b) Tambua tamathali ya usemi iliyotumiwa katika dondoo hili. (alama 2)
i) nahau- kukiangua kitendawili
ii) jazanda - neno kitendawili kurejelea jambo fulani lililofichika
c) Fafanua chanzo na hatima ya kitendawili
kinachorejelewa katika dondoo hili. (alama 10)
i)Kuwepo kwa uvumi na nong`ono kuhusu uwezekano wa kunyakuliwa ardhi ya Wanamadongoporomoka.
ii)Mzee Mago kuwahamasisha raia kuhusu haja ya kutetea kazi zao.
iii)Mikutano ya kuandaa mikakati ya kutetea haki za Wanamadongoporomoko inayofanyika katika mkahawa.
iv)Jitu kuwasili mkahawa mshenzi na kuzua taharuki
Hatima
- Jitu kuahidi kurudi keshoye kula maradufu ya siku hiyo.
i)Hatimaye jitu kufika na mabuldoza
ii)Askari wa baraza kuandamana na jitu
iii)Jeshi la polisi kuwalinda askari wa baraza
iv)Watu kupigwa virungu bila hatia
v)Vibanda kubomolewa
d) Eleza wasifu wa warejelewa katika dondoo hili. ( alama 4)
i)Wazalendo halisi; wanaendeleza harakati za kupigania haki zao za kumiliki na kukomboa ardhi yao.
ii)Wenye bidii: hawasiti /hawakomi kuandaa mikakati
ya kupigania haki zao . mfano: mikutano yao.
iii)Wenye umoja na ushirikiano : wanashirikiana kwa kukutana na kupanga utetezi wa haki zao.
iv) Wakakamavu/ jasiri: wanakaidi hatua ya Jitu na kuikomboa ardhi yao iliyonyakuliwa.
v)Wenye hekima/ busara: wanabaini hila za wenye nguvu kutaka kunyakua ardhi yao na kujiandaa kukabiliana nao.


|